Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Alireza Arafi, Mkurugenzi wa Hawza nchini Iran, katika khutuba za Swala ya Ijumaa ya jana, tarehe 10 Mehr, katika mji mtakatifu wa Qum, huku akizungumzia matukio na maadhimisho ya hivi karibuni, alisema: “Nitazungumzia kwa ufupi maadhimisho kadhaa, na baadaye katika uchambuzi wangu nitaeleza baadhi ya masuala yanayohusiana na vita vya tatu na hali ya leo. Natoa pole na rambirambi kwa kufariki kwa Marjk’ Mkuu, Ayatollah al-Udhma Shubairi Zanjani; Marji’ mkubwa ambaye alikuwa katika kiwango cha juu sana katika fiqhi, elimu za Kiislamu na elimu za Hawza, na alitoa huduma za kudumu kwenye elimu za Mwenyezi Mungu, maarifa ya Kiislamu na elimu za Hawza.”
Ayatullah Arafi aliendelea kutaja nukta tano muhimu zinazohusiana na tafiti za kimkakati na uongozi wa vita, ambazo kwa undani ni kama ifuatavyo:
1. Kusambaratika simulizi ya unafiki: Sura halisi ya Shetani Mkuu na utawala wa Kizayuni
“Kuondolewa pazia za unafiki na vinyago vinavyoonekana kuwa vya kibinadamu vya Marekani na Israel, kumefikia kiwango ambacho hata watu waliodanganywa na wajinga wameamini jambo hili, na dunia imeifahamu sura ya ndani yenye uovu ya nguvu hii ya kibeberu.”
“Huenda miaka mitatu iliyopita mtu angeweza kusema: Je, inawezekana kupatikana mchinjaji ambaye atawaangamiza watu 70,000 wakiwa majumbani mwao? Hapana; Magharibi ina sura nzuri! Hawa wanaonekana kuheshimu haki za binadamu na huko ni ardhi ya demokrasia!! Lakini vita vya hivi karibuni na mwenendo huu wa Marekani kuanzia amani na mazungumzo hadi vita, ndio uhalisia wao ulivyo.”
“Ni mara ngapi wameketi kwenye meza ya mazungumzo? Je, hawa wana mantiki ya kisheria? Unapoketi kwenye meza na kutamka sentensi fulani, huwa ina maana kubwa; lakini hawa hawakukubali maana yoyote kwa ahadi wala makubaliano yoyote. Ni mara ngapi walifikia hatua ya kusaini, kisha wakayavunja makubaliano yote waliyoyasaini! Na katika vita pia, kwa kuwaua watoto, wanafunzi na watu wasio na ulinzi, na kumuua kishahidi kiongozi na mtu mwenye shakhsia ya juu ya kidini, ambaye ni Marji’, ana uongozi na ana wapenzi wengi duniani, walimlenga kwa jeuri kubwa. Waliweka pembeni misingi yote.”
“Hii ndiyo ilikuwa sura mbaya, chafu na ovu ya ndani ya Marekani na Israel ambayo leo imekuwa wazi zaidi kuliko wakati mwingine wowote, na dunia imeifahamu hali halisi, na kauli ya ‘Mauti kwa Marekani’ haijaondolewa.”
2. Kashfa ya usaliti: Ladha chungu ya maridhiano katika kivuli cha damu za waliodhulumiwa
“Kilicho kibaya na cha kuchukiza zaidi kuliko hili ni kashfa na usaliti wa baadhi ya nchi za eneo hili katika kuungana na Marekani na Israel. Bila shaka, tulikuwa tunawajua watu kama wale wa Imarati; tulikuwa tunazijua serikali hizi ndogo, duni na zinazotegemea wengine. Hata katika miaka minane ya Ulinzi Mtakatifu, ninyi mliungana na maadui zetu, lakini daima mlidumisha mwonekano fulani; katika kipindi hiki, mapazia yote haya yameondoka na sura zao za kinafiki zimekuwa wazi.”
“Kibaya zaidi kuliko yote haya—na Mwenyezi Mungu anajua kwamba tangu nilipoona habari hii hadi sasa, moyo wangu umejaa huzuni, majonzi na hasira dhidi yao—ni kwamba katika vita ambavyo Netanyahu amewaua Waarabu 70,000, Waarabu Waislamu wa Kisunni, kwa jeuri na ukosefu mkubwa wa haya, rais huyu wa Imarati amekutana na Netanyahu. Aibu juu yenu, aibu juu yenu! Mataifa ya Kiislamu siku moja yatawawajibisha.”
“Hamumwonei haya Mtume wa Mwenyezi Mungu? Maelfu ya ndugu na dada zenu wameuawa bila hatia; leo mnasalimiana na mtu mmwagaji damu zaidi duniani, mnafanya naye mazungumzo na kufanya naye makubaliano? Ole wenu! Hatua hii ya usaliti ni miongoni mwa mambo yasiyo na mfano katika historia ya eneo hili; mambo haya yamekuwa wazi, yameandikwa na kuhifadhiwa katika kumbukumbu, na kwa wakati wake, wasaliti wa nchi za Umma wa Kiislamu wataadhibiwa.”
3. Mwisho wa “subira ya kimkakati”: Kuvunja nguvu za adui na kubadilisha mizani ya nguvu
“Kulikuwa na hofu duniani kote kuhusu kukabiliana moja kwa moja na Marekani. Dunia nzima inaogopa kukabiliana moja kwa moja na Marekani na kuingia katika meli moja nayo; na wakati mwingine Marekani ilipoingia katika uwanja fulani, wote walikwama na kujiondoa.”
“Enyi taifa kubwa la Iran! Kwa ujasiri wenu wenyewe, juhudi za viongozi wetu na kwa uongozi wa Kiongozi Mkuu, kwa utukufu na ukuu wenu huu, kwa mara ya kwanza mmeondoa hofu ya kukabiliana na Marekani na kuilenga Israel moja kwa moja, na mmeonesha kwamba sisi ni watu wa vita, tuna uwezo wa kuipinga Marekani, na kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu tutabaki juu ya ahadi na mkataba huu.”
4. Mabadiliko ya hesabu za kikanda: Kulenga mapango ya Shetani
“Kwa miaka mingi, subira ya kimkakati ya Iran ilikuwa kuzionea huruma nchi hizi zinazotumikia wengine na maeneo waliyowapa maadui zetu kambi; kuhifadhi heshima na kuzingatia desturi za ujirani, lakini hesabu hii imebadilika.”
“Kwa mara ya kwanza, Shetani Mkuu na kambi zinazoipinga Iran na Uislamu katika eneo hili zililengwa, na mpaka huu ambao tulikuwa tunauzingatia umevunjwa. Katika siku zijazo pia wanapaswa kufahamu kwamba hatua yoyote ya moja kwa moja itatulazimisha kujilinda na kushambulia mapango ya Shetani, na kamwe Majeshi yetu, chini ya uongozi wa Kiongozi Mkuu, Ayatullah Haj Sayyid Mujtaba Khamenei, hayatarejea nyuma kutoka katika mkakati huu muhimu.”
5. Kuchomoza nguvu mpya: Karata za ushindi za Iran katika uwanja wa vita
“Vita hivi vilifungua kurasa mpya, moja kati ya hizo ikiwa ni Mlango wa Hormuz na Bab al-Mandab. Katika vita hivi, jua la nguvu ya Iran na Uislamu limechomoza, jua la nguvu ya muqawama limechomoza; pia tunazo karata nyingine mpya ambazo, iwapo mtakuwa na jeuri na mkafanya mashambulizi, karata hizo mpya pia zitajidhihirisha.”
Maoni yako